Kocha wa Kihisipania Pep Guardiola anaamini James Rodriguez anaweza kufanikiwa zaidi Ligi Kuu Uingereza endapo atatua Manchester
Bosi wa Manchester United Pep Guardiola amebashiri kuwa James Rodriguez atafanikiwa kwenye Ligi Kuu Uingereza ikiwa ataondoka Real Madrid kujiunga na Manchester United.
Habari zinadai kuwa James Rodriguez ameruhusiwa kutua United baada ya habari mchanganyiko kutoka Hispania ambako amekuwa akitumiwa na Zidane kutokea benchi.
City hawamo kwenye mbio za kumwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia lakini alipoulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi dhidi ya West Bromwich Albion, Guardiola alisme kwamba mchezaji huyo hatapata tabu kulizoea soka la Uingereza.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona aliwaambia waandishi: "Kwa maana ya ubora, hakuna shaka juu yake katika Real Madrid, kwa sababu wachezaji wenzake katika kikosi hicho ni bora zaidi.
"Wachezaji wote bora duniani wanaweza kucheza ligi zote, itategemeana na timu na wachezaji wenzake, lakini ubora wake ni thabiti."
Rodriguez ameanza mechi 13 tu La Liga msimu huu, na nyingine nne katika Ligi ya Mabingwa
0 comments:
Post a Comment