![]() |
Kuondoa harufu mbaya |
Kuna dawa mmoja inaitwa Mfuleta ni dawa ya unga itokanayo na mti shamba unaoitwa mfuleta.
Dawa hii ni maarufu saana katika maduka yetu ya dawa za asili hasa
afrika mashariki. Uendapo dukani uliza tu, nataka Mfuleta muuzaji
atakupatia bei yake ni kati ya Tsh 500 mpaka 1000 kwa pakiti sawa na 0.5
USD.
MAANDALIZI
Chemsha maji safi katika chombo safi ujazo wa lita 2. Hakikisha maji yako yamechemka vizuri.
Epua chombo cha maji hayo toka jikoni, chota dawa yako ya Mfuleta vijiko 3 vikubwa vya chakula na uweke ndani ya maji hayo.
Funika chombo hicho chenye maji ya moto uliochanganya na vijiko 3 vya
Mfuleta kwa mfuniko mzuri usiopitisha hewa mpaka dawa hiyo ipowe na iwe
vuguvugu.
MATUMIZI
Tumia dawa hiyo kwa kunawia sehemu za siri kutwa mara 2. Tumia vidole vyako kuosha sehemu ya nje na ndani ya uke.
Dawa hii hutumiwa ikiwa vuguvugu kwa maana unatakiwa kuipasha joto kila siku mara tu kabla ya kutumia.
Itikise na uzungushe mkono wako katika chombo chenye dawa ili kufanya maji yachanganyikane na dawa vizuri wakati wa kunawa.
Tumia dawa hii kwa muda wa siku 30 mpaka 60 kwa matatizo yafuatayo;
1. Huondoa harufu mbaya ukeni itokayo hasa wakati wa tendo la ndoa
2. Kupunguza maji mengi wakati wa tendo la ndoa.
3. Huondoa muwasho na maji meupe au yanjano yatokakayo ukeni.
4. Husaidia kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
5. Husaidia kupunguza muda wa hedhi kwa wale wenye kupitiliza.
ZINGATIA
Mfuleta ni dawa ya unga yenye rangi ya weupe, ukiilamba ladha yake ni ya
muwasho kidogo kama pilipili, ukitia katika tundu za pua itakufanya
upige chafya.
SOURCE:
1 comments:
MWAMBUNGU hapa Mkoa gani Hiyo Dawa inapatikana kwa Wingi?
Post a Comment