Pages

Subscribe:

Tuesday, 16 May 2017

Antonio Conte amefaidi jasho la Jose Mourinho

Antonio Conte amefaidi jasho la Jose Mourinho
Mourinho kila anakopita huunda kikosi bora na anapoondoka wanaokuja nyuma yake wanapata mafanikio bila kutumia nguvu, Conte amesafiria nyota yake

Antonio Conte amefanikiwa sana akiwa na timu ya Chelsea kwa mara ya kwanza msimu, ni baada ya kuitwaa timu hiyo iliyokuwa ikinolewa na kocha wa Manchester United Jose Mourinho.
Antonio Conte hakuwa na mabadiliko ya kufanya kwenye kikosi hicho kilichoibuka mabingwa wa ligi zaidi ya kumsajili N'Golo Kante katika kikosi chake na kubadilisha mfumo wa uchezaji wa timu.
Kikosi alichopata Conte ndicho kilichomwezesha kutwaa ubingwa, licha ya uwezo wake wa kimbinu na kubadili mfumo, Jose Mourinho ndiye aliyeunda kikosi thabiti na kukiacha baada ya kushindwa kuwa na maelewano mazuri na wachezaji hadi kufukuzwa kazi.
Mchambuzi wa masuala ya soka Garry Neville anaona Conte anafaidi matunda ambayo yalipandwa na Jose Mourinho kutokana na aina ya kikosi ambacho Mourinho alikiacha.
“Hii sio mara ya kwanza kwa Mourinho kutengeneza kikosi bora halafu akawaachia wanaofuata wafaidi, alifanya hivyo kwa Ancelotti na sasa hata Conte anafaidi kikosi kilichoachwa na Mourinho” alisema Neville.
Lakini Neville anaona Conte msimu ujao atakuwa na wakati mgumu zaidi akitaja mambo matatu amabyo yatampa tabu Muitaliano huyo msimu ujao.
Moja kati ya mambo hayo ni uthabiti wa kiuchezaji, Neville anaona Chelsea msimu ujao wachezaji wanaweza kuwa wamechoka kutokana na kazi kubwa waliyofanya msimu huu hali kadhalika watakuwa na michuano mingi.
Neville anaamini kuwepo katika mashindano machache kumechangia Conte kufanya vizuri msimu huu, changamoto ya pili ni utimamu wa kiakili kwa wachezaji wa Chelsea.
“Wachezaji hawa hawa ndio ambao walichukua kombe na Mourinho na kisha msimu uliofuata wakaanguka, sio rahisi wakawa na uthabiti wa kushinda kila msimu na hilo pia linanipa mashaka” alisema Neville.
Changamoto kubwa nyingine ambayo Neville anaamini itawasumbua Chelsea ni Diego Costa ambaye hana uhakika wa kubaki klabuni hapo, na kama akiondoka Neville analiona kama tatizo kubwa Chelsea.

0 comments:

Post a Comment