Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza
mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’
aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’,
Risasi limenyetishiwa ubuyu.
Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa
hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah
alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari
alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.
“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa
watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee
haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa
habari huyo na kuongeza:
“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”
Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa
Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa
na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa
kujifungua Desemba, mwaka huu.
Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu
alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao
ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.
“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua
Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina
uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.
chanzo:gpl
0 comments:
Post a Comment