![]() | ||
Mwewe (Eagle) |
kwa lugha ya kingereza ni maarufu kwa jina la Eagle.
![]() |
Mwewe ni ndege maarufu kwa tabia yake ya uwindaji |
Ukiwa umelala ukaota ndoto unamuona ndege aina ya Mwewe akiwa juu ya mti
au kitu chochote chenye urefu mara mbili yako, pia sehemu alipo haguswi
na mwanga wa jua na wala hatoi sauti kabaki tu kukuangalia na nafsi
yako ina wasi wasi au khofu.
Ndoto hiyo ina maana ya uadui wa kijicho kutoka kwa mtu lakini wewe bado hujamjua ni nani.
Anaweza kua ni mtu wa karibu yako au laa. Lakini ni mtu ambae anaweza kua ni mwenye madhara makubwa kwako.
Ndoto hiyo inakutaka kuchukua tahadhari na neema yoyote uliyonayo hata kama katika macho yako utaiona duni vipi.
Pia chagua marafiki wema katika kusuhubiana nao na uwatendee watu kwa namna iliyo bora.
0 comments:
Post a Comment