Pages

Subscribe:

Thursday, 19 October 2017

CHELSEA YAKAMATWA DARAJANI NA ROMA, MANCHESTER UNITED IKISHINDA UGENINI...Matokeo ya mechi zote yako hapa


Chelsea wamepona kwenye vita kali dhidi ya Roma kupata sare ya 3-3 Ligi ya Mabingwa Darajani Stamford, United, Barca, Bayern, PSG na Juve zikishinda

Chelsea 3-3 Roma

Chelsea wamepona kwenye vita kali dhidi ya Roma kupata sare ya 3-3 Ligi ya Mabingwa Darajani Stamford.
Miamba hao wa Ligi Kuu Uingereza waliongoza kupitia goli la David Luiz na Eden Hazard, lakini Aleksander Kolarov na magoli mawili kutoka kwa Edin Dzeko yalipindua mechi yote London.
Eden Hazard Chelsea
Hata hivyo, bao la kichwa la Hazard dakika ya 15 kabla ya mechi kumalizika liliwahakikishia Chelsea kubaki kileleni mwa Kundi C, na pointi tano mbele ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya tatu.
Mabao ya As Roma yeliwekwa kimiani na Aleksandre Kolarov na Eden Dzeko aliyefunga mara mbili na kumfanya Antonio Conte kwa mara ya kwanza kuruhusu mabao 3 katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa.

Barcelona 3-1 Olympiakos Piraeus

Barcelona wamepiga hatua kubwa kuelekea kufuzu hatua ya 16-Bora kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Olympiakos katika uwanja wa Camp Nou licha ya kulazimika kucheza wakiwa kumi.
Lionel Messi Barcelona
Lionel Messi alifunga bao lake la 100 katika michuano ya soka Ulaya wakati Barcelona wakiifunga Olympiakos mabao 3 kwa 1 huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na Nikolaou na Lucas Digne, huku Gerrad Pique akipewa kadi yake nyekundu ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa.

Bayern Munich 3-0 Celtic

Bayern Munich walijipatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Celtic usiku wa Jumatano na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi B Ligi ya Mabingwa.
Thomas Muller Bayern 2017
Klabu hiyo ya Scotland ilitua Allianz Arena ikiwa imetoka kushinda ugenini dhidi ya Anderlecht lakini ilizidiwa kila kitu na Bayern mpya ya Jupp Heynckes.
Magoli kutoka kwa Thomas Muller na Joshua Kimmich yaliiwezesha Bayern kuongoza kipindi cha kwanza na Mats Hummels akaongeza lingine kipindi cha pili.

Juventus 2-1 Sporting CP

Juventus walitoka nyuma ya bao moja na kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Sporting Cp huku mabao ya Juventus yakiwekwa kimiani na Stefanl Sturalo huku la ushindi likiwekwa kimiani na Mario Mandzukic.

Anderlecht 0-4 PSG

Edinson Cavani Kylian Mbappe Anderlecht PSG UEFA Champions League 18102017
Paris Saint German waliibuka kidedea kwa mabao 4 kwa nunge huku Kylian Mbappe, Edson Cavanni,Neymar na Di Maria wakifunga na goli la Cavanni likamfanya kuwa mchezaji wa 3 kufunga katika michezo 7 mfululizo katika Champions League baada ya Niestrooy na Cr7.

Benfica 0-1 Manchester United

Douglas Marcus Rashford Benfica Manchester United
Matokeo mengine Manchester United waliichapa Benfica bao 1 kwa sifuri bao la Marcus Rashford, Bayern Munich wakawapiga Celtic 3 kwa nunge, Athletico Madrid na Quarabag Fk wakaenda sare ya bila kufungana.

0 comments:

Post a Comment