Pages

Subscribe:

Sunday, 15 October 2017

Ndege ya mizigo yaanguka baharini Ivory Coast


Mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika.
Ndege moja ya mizigo imeanguka katika bahari ya taifa la Ivory Coast , muda mfupi baada ya kuondoka mji mkuu wa Abidjan huku watu watatu wakidaiwa kufariki na wengine wakijeruhiwa.

Mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika.
Ndege hiyo ilikuwa ikibeba mizigo ya jeshi la Ufaransa, kulingana na duru za mtandao wa Koaci.
Inasemekana kuanguka wakati wa mvua kubwa karibu na bandari ya Bouet.
Ramani ya taifa la Ivory Coast
Image captionRamani ya taifa la Ivory Coast
Shahidi mmoja ameambia chombo cha habari cha Reuters kwamba watu wanne walifariki: miili miwili ikitolewa kutoka kwa ndege hiyo huku mingine miwili ikionekana katika mabaki ya ndege hiyo.
Lakini vyombo vya habari na tovuti ya Ivoire Matin iliripoti vifo vya watu watatu huku watu sita wakijeruhiwa.
Mtu mmoja amekamatwa, kimeongezea.
Mabaki ya ndege hiyo yako katika ufukwe wa bahariniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMabaki ya ndege hiyo yako katika ufukwe wa baharini
Kulingana na mtandao huo , watu 10 walikuwa wameabiri ndege hiyo wakati ilipoanguka.
Ndege hiyo imedaiwakutengezwa nchini Ukrain.

0 comments:

Post a Comment