Pages

Subscribe:

Thursday, 19 October 2017

NEYMAR AAHIDI KUMSAIDIA MBAPPE KUWA SUPASTAA WA PSG... KAMA ALIVYOFUNDISHWA NA MESSI BARCELONA


Nyota huyo wa Kibrazili anataka kumsaidia mchezaji mwenzake kama yeye alivyosaidiwa na supastaa wa Barcelona mwanzoni akiwa Camp Nou
Neymar anataka kuwa msaada kwa Kylian Mbappe katika klabu ya Paris Saint-Germain, kama Messi alivyomsaidia Mbrazili huyo alipokuwa Barcelona.
Mshambuliaji huyo na mchezaji mwenzake kinda wote walizifumania nyavu PSG iliposhinda 4-0 dhidi ya Anderlecht kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa, Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 18 akifunga dakika tatu tu baada ya kumtengea Edinson Cavani kufunga na kuiwezesha timu yake kuongoza kwa 2-0 kipindi cha kwanza.
Neymar alifumania nyavu baada ya saa moja kwa mpira wa dhabu ndogo kabla ya Angel Di Maria kufunga ukurasa wa mabao dakika za majeruhi.
Goli la Mbappe, la nane kwenye michuano hiyo, limemfanya kuwa kinda mwenye magoli mengi kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa, na klabu yake imekuwa na mwanzo mzuri msimu huu baada ya kushinda mechi 11 kati ya 12 kwenye Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa.
Wakati dalili zikiwa nzuri kwa safu ya mashambulizi ya PSG, Cavani akifikia anga adimu kwa kufunga goli lake la saba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alidokeza kuwa hakuna utulivu kwenye kikosi hicho kuelekea mechi ya Jumatano kwa kudai kuwa wachezaji nyota hawana ulazima wa kuwa marafiki.
Licha ya kauli yake, Neymar ameweka bayana baada ya mechi kuwa hahitaji kuwa na urafiki, angalau akiwa na mchezaji mwenzake kinda, akidai angependa kumsaidia Mbappe kama Messi alivyomsaidia yeye.
"Ningependa kumtendea Mbappe kama vile Messi alivyonitendea mimi," alisema kupitia Brazilian TV.
"Nataka kumsaidia. Ni rafiki yangu kipenzi."
PSG watarejea mzigoni kwa safari ya Ligue 1 kwenda Marseille Jumapili.

0 comments:

Post a Comment