Akishiriki hafla ya shukrani iliyoandaliwa na mbunge mwanamke wa Namutumba Mariam Naigaga Jumatatu, Rais Museveni alisema hatavumilia tena vitisho kutoka kwa upinzani.
"Ninataka kuwaonya wale wote ambao wanawatishia watu, (akabwa akasiru kayigga enjovu) mbwa mpumbavu humwinda tembo)... kwa kufikiri kwamba mnaweza kuitishia NRM, na mnatumia vurugu, nasema bado NRM ni bingwa wa vurugu lakini vurugu zetu zina nidhamu na zenye lengo,” Museveni alizungumza kwa ukali.
“Nataka kuwashauri kuwa mtu yeyote mwenye ndoto kuwa anaweza kufanya vurugu na kuwanyamazisha (watu wetu); hatutapoteza muda wetu,” alisema Museveni.
Rais Museveni alizungumza hayo baada ya mashambulizi ya ghafla dhidi ya wabunge wa NRM. Miongoni mwa walioshambuliwa na umma wenye hasira ni Simeo Nsubuga (Kassanda Kusini), James Kakooza (Kabula), Ibrahim Abiriga (Manispaa ya Arua), Judith Nabakooba (Wanawake wa Mityana), Doreen Amule (Amolatar) na Godfrey Kiwanda Ssuubi (Mityana Kaskazini).
Waziri wa Nchi wa Maendeleo Mijini Isaac Musumba (Buzaaya) na Connie Nakayenze Galiwango (Wanawake Mbale) wameshindwa kuyashawishi majimbo yao kuunga mkono kuondolewa kwa ukomo cha umri.
Dunia ilishuhudia matukio ya ghasia katika Bunge Septemba 26 na 27, wakati ngumi zilipofumuka muda mfupi baada ya waziri mdogo Ronald Kibuule kudaiwa kuingia na bunduki ndani ya Bunge. Museveni alitoa wito wa majadiliano yenye utulivu.
"Suala hili lijadiliwe kwa utulivu, kwa upole…hakuna haja ya kutukuna, toa hoja zako; huna haja ya kumtisha yeyote ili kufikia suluhisho sahihi,” alisema Museveni.
0 comments:
Post a Comment