Palace wamefanikiwa kupata alama tatu kwa mara ya kwanza na kufunga goli lao la kwanza kwenye msimu huu, baada ya kuibuka na ushindi dhidi Chelsea
Palace walichukua uongozi baada ya dakika ya 11 kufuatia krosi ya Andros Townsend kumkuta Yohan Cabaye ambaye aliupiga mpira na kumngonga Cesar Azpilicueta kabla ya kuingia kwenye wavu, na kusababisha furaha kutoka kwa timu hiyo ya nyumbani.
Chelsea walisawazisha goli hilo ndani ya dakika saba, kona ya Cesc Fabregas kutoka upande wa kulia ambayo ilishindwa kuokolewa vyema na Watford na kuruhusu Tiemoue Bakayoko ambaye hakuwa amekabwa kufunga goli lake kwa la kwanza la Ligi Kuu.
Dakika chache baadae Chelsea kisha walimpoteza Victor Moses kwa kuumia nyama za paja, na kuafanya nafasi yake kuchukuliwa na Davide Zappacosta katikati ya nusu ya kwanza ya mechi, matatizo ya wageni (Chelsea) yaliongezeka kufuatia Wilfried Zaha kufunga la pili.
Mamadou Sakho aliifanya kaz nzuri kwa kupanda hadi mbele na kufanikiwa kunyang'anya mpira na kumpa nyota mwenzake, Zaha ambaye hakufanya makosa, kufuatia kumchungulia Thibaut Courtois alivo kaa na kumpelekea kona ya chini ya kulia.
Pande zote mbili zilishambuliana kwa zamu katika kipind cha pili, ila Palace wata jirahumu kutokana na kupoteza nafasi nyingi za walizoshindwa kuzitumia vizuri na wachezaji wake.
Dakika za mwisho kidogo Sakho aizawadie Chelsea goli kufuatia makosa yake ya dakika za mwisho akijaribu kuokoa hatari kwa staili ya kisigino lakini mpira uliishia karibu na kumkuta Fabbregas ambaye shuti lake chupu chupu litinge nyavuni.
Ushindi wa Palace bado umemfanya asalie nafasi ya 20 kwenye msimamo wakati Chelsea sasa wako nyuma kwa pointi tisa dhidi ya vinara wa ligi Manchester City.
0 comments:
Post a Comment