Mchezaji wa kimataifa wa Argentina amecheza mechi yake ya kwanza tangu Septemba alipopata ajali ya gari Amsterdam, na ameifikia rekodi ya Eric Brook ya magoli 177 baada ya Bernardo Silva kuangushwa na mlinda mlango Nick Pope dk ya 30.
Vinara hao wa Ligi Kuu Uingereza walilazimika kufanya kazi ya ziada Etihad kufuatia usumbufu wa Burnley, lakini magoli mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Nicolas Otamendi dk 73 na Leroy Sane dk 75 yalivunja nguvu za Burnley.
City wameweka rekodi ya kushinda mechi 11 mfululizo katika michuano yote, pamoja na kipigo cha 2-1 cha Manchester United ugenini dhidi ya Huddersfield inamaanisha timu ya Pep Guardiola imewaacha mahasimu wao pointi tano na kujikita kileleni.
Kwa upande mwingine, Burnley, ambao wamempoteza kinara wao wa mabao Chris Wood kwa majeraha mapema kipindi cha kwanza, wanashika nafasi ya tisa baada ya kipigo cha kwanza cha ligi tangu Agosti 19.
Baada ya kushinda dhidi ya Chelsea na kupata sare nzuri Anfield na Wembley, Burnley walipata pigo la majeraha ya Wood, yanayohofiwa kuwa ni misuli ya paja.
Pigo hilo liliongezeka uzito baada ya mwamuzi Roger East kutoa adhabu ya penalti dhidi ya Pope kwa kumchezea rafu Silva, na kumruhusu Aguero kufunga kwa tuta.
Sergio Aguero (177), amekuwa mchezaji wa pili kufunga magoli mengi muda wote klabuni sambamba na Eric Brook.
City wanapewa nafasi kubwa kusonga hatua ya robo fainali Kombe la Carabao watakapoikaribisha Wolves katika uwanja wa Etihad Jumanne, kabla ya kurejea kwenye mechi za ligi dhidi ya West Brom Oktoba 28.
Burnley watacheza dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Turf Moor mechi inayofuata
0 comments:
Post a Comment