Siku moja baada ya kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, kuamua kujiuzulu kuifundisha timu hiyo kocha mkuu wa Yanga Mzambia George Lwandamina, amesema zamu inayofuata kwasasa ni ya kocha mkuu wa wapinzani wao wa jadi Simba Joseph Omog.
Lwandamina ameiambia Goal , pamoja na Mayanja, kuondoka niwazi kuwa hali si shwari ndani ya timu hiyo na mlengwa mkubwa ni Omog, hivyo atahakikisha anakamilisha safari yake mapema Oktoba 28, wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
"Kuondoka kwa Mayanja siyo mwisho wa matatizo ya Simba, tatizo kubwa lililopo pale ni kocha mkuu ambaye bado hajathibitisha uwezo wake na hilo tutalidhihirisha sisi Yanga kwenye mchezo wetu wa Oktoba 28 pale uwanja wa Uhuru," amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mcheozo huo na hiyo ni kutokana na kuimarika kwa kikosi chake katika kila mchezo ambao wamekuwa wakicheza hivi karibuni ndiyo maana anauhakika wa kupata matokeo katika mchezo huo.
Amesema anajua kuwa Simba ni timu yenye kikosi bora, lakini kukosa kocha mwenye uwezo na mbinu bora ndiyo kinachompa matumaini ya kushinda mchezo huo ambao wamepania kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kutwaa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.
Yanga ipo mkoani Tabora, ambako jana ilicheza mechi ya kirafiki na Rhino Rangars, na kutoka sare ya bila kufungana na inajiandaa na mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Stand United ambao utapigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment