Manchester United na Huddersfield watakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 45.
Vijana wa Jose Mourinho watakuwa ugenini wikendi hii kuwakabili timu iliyopanda darajia msimu huu, Hudderfield katika uwanja wa John Smith's, mechi inayotarajiwa kufanyika majira ya saa kumi na moja majira ya Afrika Mashariki.
Taarifa Muhimu kuhusu timu
Marcus Rashford ambaye alitolewa dakika za mwishoni dhidi ya Benfica, baada ya kufunga goli pekee lililowapa ushindi Mashetani Wekundu siku ya Jumatano, Mourihno amethibitisha kuwa nyota huyo wa Uingereza yupo fiti kwa ajili ya mechi hiyo, pia mwalimu huyo amesema itakuwa ni vigumu kwa Erick Bailly kurejea siku ya Jumamosi na kuna mashaka pia kwa Fellaini na Pogba kuhusu mechi dhidi ya Hudderfield, Marcos Rojo na Ibrahimovic wanaendelea kuimarika taratibu
Huddersfield watawakosa nyota wake kadhaa kama Michael Hefele, Jon Gorenc-Stankovic, Kasey Palmer na Philip Billing huku washambuliaji wake Steve Mounie na Collin Quaner watarejea kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu.
Fomu ya Huddersfield kwa msimu huu
Vijana wa David Wagner waliuanza msimu wa Ligi Kuu kwa kishindo baada ya kuifunga Crystal Palace mabao 3 kwa 0, na kuifunga tena Newscastle goli moja kwa bila baada ya ushindi wa mechi hizo mbili, Terries wameshindwa kuibuka na ushindi katika mechi 6 na wataingia kwenye mechi hiyo dhidi ya United huku wakihofia kufungwa mechi ya tatu mfululizo kufuatia kupoteza mechi ya Swansea na Tottenham.
Mechi walizokutana
United wanarekodi nzuri dhidi ya Terries, wameshinda mechi 20 kati ya 45, sare 10 na Huddersfield wakiibuka na ushindi wa mechi 10, cha kufuraisha klabu hizi mbili hazijawahi kukutana tangu msimu wa mwaka 1971/1972.
Mwamuzi wa Mechi hii
Lee Mason anatarajiwa kuwa refarii wa mchezo huo huku akisawadiwa na Harry Lennard na Matthew Wilkes
0 comments:
Post a Comment