Pages

Subscribe:

Thursday, 19 October 2017

FASTA SIMBA YAMTANGAZA MRITHI WA MAYANJA


Ikiwi ni masaa machache tangu kutangaza kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Jackosn Mayanja Simba imemtangaza Masud Juma kuziba nafasi yake
Hatimaye klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi kocha Masud Juma, kuwa mrithi wa kocha Jackson Mayanja, ambaye jana alitangaza kujiuzulu kuhudumu kwenye timu hiyo kutokana na mambo ya kifamilia ambayo yanamkabili.
Masud raia wa Burundi ameiambia Goal, wakati wa utambulisho huo kuwa anafurahi kutua Simba, katika nafasi ya kocha msaidizi, na kinachomfanya kufurahi ni kwa sababu hiyo ni timu kubwa Afrika Mashariki na Kati na atahakikisha anashirikiana vyema na kocha mkuu Joseph Omog, ili kuendeleza malengo ambayo wamejiwekea kwa msimu huu na inayokuja.
"Nafurahi uongozi wa Simba kuniamini na kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangu kuifundisha timu yao niseme tu kwamba nipo tayari kushirikiana na viongozi, kocha mkuu Joseph Omog, pamoja na wachezaji lakini siku zote nitahakikisha nafanya kazi kwa uwezo bila kuogopa kufukuzwa," amesema Juma.
Kutia saini ya mwaka mmoja kuifundisha Simba kuna maliza uvumi ambao awali ulikuwa ukimuhusisha kocha huyo kujiunga na vinara hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba pamoja na kocha wa Lipuli ya Iringa Selemani Matola.
Juma anakuwa kocha wa tatu raia wa burundi kufundisha timu za Ligi Kuu ya Tanzania wengine ni Ettiene Ndayiragije wa Mbao FC na Ramadhani Nsanzurwimo ambaye kama mambo yataenda sawa huenda akajizolea umaarufu kama ilivyo kuwa kwa Ndayiragije.

0 comments:

Post a Comment