Mourinho mwenye umri wa miaka 54 amedai kuwa yupo tayari kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Old Trafford baada ya kushinda mataji mawili katika kampeni zilizopita.
Kocha huyo ambaye ameshazinoa klabu tofauti-tofauti katika miaka 17 kama meneja, anaamini kuwa kudumu Old Trafford robo karne kama Sir Alex Ferguson ni jambo ambalo haliwezi kuwa na uhalisia.
"Jambo pekee ninaloweza kusema ni kwamba mimi bado ni kocha mwenye hofu, mwenye malengo, shauku ya kufanya mambo mapya," aliwaambia Telefoot. "Nina uhakika sitamaliza muda wangu hapa [Manchester] kama kocha."
Mourinho anakaribia kugawa nusu ya mkataba wake wa miaka mitatu aliosaini alipochukua mikoba ya Louis van Gaal Mei 2016.
0 comments:
Post a Comment