Mserbia huyo alitamka kuwa uwepo wa Mourinho Man United ndio uliomfanya aamue kutua Old Trafford majira ya joto.
"Mourinho ni mtu wa kipekee, na kocha bora niliyewahi kufanya naye kazi," kiungo huyo mkabaji alisema. "Wakati mwingine si rahisi kufanya naye kazi, kwa sababu anahitaji kazi zaidi.
"Hata unapocheza katika kiwango cha juu zaidi katika mechi, anakutaka ucheze zaidi mechi inayofuata."
Matic anaendelea vizuri chini ya Mourinho baada ya kutua United kwa paundi milioni 35, na ameendeleza ubora wake katika safu ya kiungo United wakiifunga Benfica 1-0 Ligi ya Mabingwa Jumatano.
Wawili hao walitwaa taji Ligi Kuu Uingereza miaka miwili iliyopita wakiwa Chelsea na Matic bado anamsifia meneja wake.
"Kiuhalisia ni mtu tofauti kabisa na anavyochukuliwa na umma wote," alisema. "Ni mtu mwenye sifa zote za kibinadamu. Si mtu yule anayezungumziwa tofauti kwenye vyombo vya habari.
"Ameunda kundi bora la wachezaji wenye uwezo, na tunakila kitu cha kutuwezesha kupata matokeo mazuri."
0 comments:
Post a Comment