Pages

Subscribe:

Sunday, 15 October 2017

MANENO YA KLOPP KWA MOURINHO BAADA YA SARE YA BILA KUFUNGANA JANA


Bosi huyo wa Kijerumani alivurugwa na mbinu walizotumia United katika uwanja wa Anfield na kumtaka meneja mwenzake kuacha mchezo huo
Jurgen Klopp ameziponda mbinu za Jose Mourinho wakati Manchester United ikipata sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool Jumamosi.
United kwa kiasi fulani walicheza kwa kujihami mechi hii, mshambuliaji Romelu Lukaku akigusa mpira mara 22 tu dakika zote alizocheza.
Liverpool walipiga mashuti 19 na walitawala zaidi mchezo lakini hawakuweza kuona nyavu mbele ya David de Gea.
Muhispania huyo aliokoa mchomo hatari kutoka kwa beki wa Liverpool Joel Matip kipindi cha kwanza, akiutoa mpira kwa miguu yake.
Na Klopp alieleza kukerwa kwake baada ya mechi.
"Kwa hakika hatuwezi kucheza namna hii Liverpool, lakini ilikuwa sawa kwa Manchester United," alikiambia Sky Sports.
"Manchester United walikuja kuchukua pointi moja na wameipata. Tulitaka pointi tatu na hatukuzipata."
Jurgen Klopp Liverpool
Liverpool sasa wamepata sare katika mechi zao tatu za mwisho kwenye michuano yote, lakini Klopp anaamini timu yake itaonyesha ubora wao wiki chache zijazo.
"Hadi sasa tumepoteza mechi moja tu Ligi ya Uingereza. Kila mmoja anaweza kuona hatupo mbali sana na Manchester United. Nadhani vijana wangu wamefanya vizuri," aliongeza.
"Tunahitaji kukitafakari kiwango chetu na hali yetu baada ya mechi hii, si kibaya. Tulitaka kushinda na kila mmoja aliweza kuona hilo.
"Kulikuwa na jitihada binafsi kutoka kwa wachezaji wetu, lakini mambo yalikuwa magumu kwetu.
"Tulilazimika kuongeza jitihada zaidi lakini tumeambulia pointi moja. Tunahitaji bahati."

0 comments:

Post a Comment