Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi
wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara
ya kumpongeza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, akitokea Marekani alikokuwa
akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na Raisi Obama.
SHANGWE ilitawala wakati
mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016
akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka
Bara la Afrika.
Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline,
ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo
aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama.
Akizungumza na wanahabari, Geline
alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa
Kanzidata ya Katiba litakuwa wazo kubwa ambalolitakubalika mpaka na
Rais Obama.
Hata hivyo Geline alisema amefurahishwa na program hiyo ya Mandela Washington Fellowship kwani imewawezesha washiri kikujifunza mambo mengi na kupata uono mpana zaidi wakufanya mambo.
Geline iliwahimiza watanzania
kutembelea Kanzidata hiyo iliyopo mtandaoni
(http://katiba.humanrights.or.tz/) ili kuweza kuijua katiba yao na
kuweza kujua haki zao kama watanzania.
Mwisho alishukuru wa mapokezi makubwa ambayo pia hakuyatarajia.
Akitoa neno la shukurani kwa Geline
kwa niaba ya LHRC, Mkurugenzi wa Fedha naUtawala-LHRC, Ezekiel Masanja
amempongeza Geline kwa kuitoa kimasomaso LHRC na Tanzania kwa ujumla.
Geline Fuko amepata kutambulika baada
ya Rais Obama kumtaja kama mfano wa kuigwa wa wanaharakati wa haki za
binadamu wakati akizungumza Jumatano Agosti 3, 2016 katika kilele cha
mpango wake wa kuwawezesha vijana wakiafrika unaojulikana kama Mandela
Washington Fellowship.
Raisi Obama alimsifu mwanasheria huyo kutoka LHRC ambaye ni moja ya vijana 1000 waliokuwa jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo ili kuweza kusaidia Maendeleo katika Nyanja zote za maisha katika nchi zao.
RaisiObamaalisifujuhudizaGelinezakuibuawazo
la kuanzishakwamaraya kwanza Kanzidata ya Katiba nchini Tanzania kwa
kutekeleza wazo hilo chiniya LHRC.
Raisi Obama alikaririwa akisema Marekani itaendelea kushikamana na wanaharakati kama Geline Fuko kutoka Tanzania.
GelinenimwanasherianamwanaharakatiwahakizabinadamuambayeamefanikishakuanzishwakwaKanzidatayaKatibaya
kwanza nayapekeenchini Tanzania inayowawezesha watanzania kusoma Katiba
kupitia simu zao za mkononi”.
Programu ya Mandela Washington
Fellowship yenye lengo la kuwa wezesha vijana wa Kiafrika katika Nyanja
za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kijamii ilianzishwa na Rais Obama
mwaka 2014.
Programu hii hujumuisha vijana elfu
moja (1000) kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao hugharamiwa na
serikali ya Marekani kwenda jijini Washington kwa lengo la kujengewa
uwezo zaidi.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzisha Kanzidata ya Katiba mwaka mmoja uliopita mnamo Julai 15, 2015.
Kupitia tovuti maalumu
(http://katiba.humanrights.or.tz/) na simu za mkononi, watanzania
wanaweza kusoma Katiba katika Kanzidata hiyo.
source: Gpl
0 comments:
Post a Comment