KUFUATIA
mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu
wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa
kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka
wahusika wote kujisalimisha.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi
limehusisha tukio hilo na kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta
Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao
wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao
wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la
Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi
wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi
yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya
ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa
watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
“Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani” amesema.
Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa
ikitumika kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na
kufanya mapambano na jeshi la polisi

“Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani” amesema.
Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.
“Katika tukio hilo majambazi ambao
idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbili aina ya MSG na
lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa,
ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la
kuwashambiulia askari polisi, ” alisema.
Alisema katika hali ya kushangaza
baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.
source:gpl
0 comments:
Post a Comment