UNAWEZA
usiamini; waziri mkuu wa nchi anauawa mitaani akiwa anatembea kwa miguu
kutoka ukumbi wa sinema na mkewe!
Hilo lilitokea miaka 30 iliyopita
wakati wasomaji wengi wa safu hii walikuwa hawajazaliwa ama walikuwa
watoto wadogo.
Aliyeuawa alikuwa ni Olof Palme (majina yake kamili yakiwa ni Sven Olof Joachim Palme aliyekuwa Waziri Mkuu wa Sweden.
Palme alikuwa ni mmoja wa marafiki
wakubwa wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hii, Julius Nyerere na rafiki
mkubwa wa mamilioni ya walimwengu waliokuwa wanapiga vita ukoloni,
umaskini na kutetea amani kwa watu wote wenye fedha na wasiokuwa na
fedha. Aliamini binadamu wote walistahili kufurahia kila alichokiweka
Mungu duniani.
Alishutumu waziwazi uonevu wa mataifa
makubwa dhidi ya mataifa madogo uliokuwa ukiongozwa na Marekani na Urusi
ya Kikomunist. Aliyalaani kwa majina mataifa makubwa yaliyokuwa
yanaanzisha vita kwa ajili ya kujinufaisha.
Kwa kifupi, alikuwa ni rafiki mkubwa wa
Waafrika na maskini wengine waliojaa katika kona mbalimbali za dunia.
Pendo la walimwengu kwake linaweza likalinganishwa tu na lile alilokuwa
anapewa aliyekuwa kiongozi wa Afrika Kusini, marehemu Nelson Mandela.
Palme aliyezaliwa Januari 30, 1927,
aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu ambaye hajajulikana mpaka leo na lengo
lake likiwa halijajulikana pia. Mpaka leo walimwengu wanajiuliza Palme
alikuwa amekosa nini hadi kuadhibiwa kwa ‘mtindo’ huo. Ni kitendawili
kinachoendelea mpaka leo.
Pamoja na wema wake wote huo, Palme, mume wa Lisbet Palme na aliyekuwa kiongozi wa Democratic Party, aliuawa usiku wa Februari 28, 1986 kwa kupigwa risasi kutoka nyuma na mtu aliyekuwa karibu nao, yeye na mkewe. Risasi ya pili ililengwa kwa mkewe, Lisbet, lakini bahati ilimkwangua mgogoni, akanusurika japokuwa ilimuumiza vibaya.
Ifahamike kwamba viongozi wa nchi za Nordic yaani Sweden, Norway na Finland huwa hawatii maanani sana kuwa na walinzi wakiamini nchi zao ni za wastaarabu na zenye amani.
Ndivyo alivyotoweka Olof Palme, kiongozi
aliyekuwa na taswira ya kuvutia na kipenzi cha ‘malofa’ duniani,
ambapo hadi leo hakuna aliyekamatwa kwa kumuua na kwa sababu ipi!
source: gpl
0 comments:
Post a Comment