Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa
mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam
ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.
Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com
na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake
na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya
huko Bagamoyo Pwani.
Sasa leo Agosti 6, 2016 tumepata taarifa
nyingine kwamba staa huyo kahamishwa kutoka Sober House ya Bagamoyo na
kuhamishiwa Sober House ya wanawake tu walioathirika na madawa ya
kulevya iliyopo Kigamboni.
Mmiliki wa kituo hicho Nuru kayaongea haya..>>>>>Mimi
naitwa Nuru ni mmiliki wa Sober House ya wanawake tu iliyopo Kigambo
juzi tulipata ugeni kutoka kwa Msanii Ray C alikuja kuomba matibabu
kwasasa yuko anaendelea vizuri na amekubaliana na hali yake’- Nuru
‘
Tumempokea vizuri na yeye
mwenyewe amefarijika sana kiufupi tu mashabiki wake wamuombee dua sana
na mpaka sasa hivi afya yake inaendelea vizuri’- Nuru
source:milardayo.com
0 comments:
Post a Comment