Mchoro: Uzito wa sayari hiyo unadokeza huenda ikawa na mawe kmaa ailivyo Dunia
Wanasayansi
wamegundua sayari ambayo inakaribia sana Dunia kwa mazingira na ukubwa
wake na ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri, iliyo
na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.
Kifaa cha HARPS kiliwekwa kwenye darubini ya 3.6m katika kituo cha kufuatilia anga za juu La Silla, Chile
Sayari hiyo, ambayo kwa sasa imepewa
jina ‘Proxima b’ inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezekano
mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.
Proxima inapatikana umbali wa kilomita
trilioni 40 na inaweza kumchukua mtu, akitumia teknolojia ya sasa ya
vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko.
Njia mpya zinazofikiriwa za kurahisisha usafiri ni kutumia teknolojia ya laser
Licha ya kwamba ni mbali sana,
kugunduliwa kwa sayari hiyo huenda kukasisimua hisia na mawazo ya
binadamu na wanasayansi kuhusu kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine
au uwezekano wa wakati mmoja watu kuishi kwenye sayari nyingine.
Proxima Centauri inavyoonekana kwa kutumia darubini ya Hubble Space Telescope
“Kusema kweli, kufika huko kwa sasa hiyo
ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria
hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja huenda watu
wakatuma chombo huko,” Guillem Anglada-Escudé, ambaye kundi lake la Pale
Red Dot limechapisha matokeo ya ugunduzi wa sayari hiyo
katika jarida
la Nature amesema
Mapema mwaka huu, bilionea Yuri Milner
alisema atawekeza $100m katika utafiti wa kuunda chombo au kifaa kidogo
kinachoweza kusafiri anga za juu kwa kutumia teknolojia ya laser.
Chombo
kama hicho kinaweza kusafiri kwa pengine asilimia 20 ya kasi ya mwanga
na hivyo kufupisha safari ya kufika kwenye nyota kama vile Proxima
Centauri kutoka maelfu ya miaka hadi miongo kadha.
Ugunduzi wa sayari hiyo ulifanikishwa kupitia darubini ya kisasa yenye kifaa kujulikanacho kama HARPS.
Darubini hiyo imewekwa nchini Chile.
Takwimu
kutoka kwa darubini hiyo zinaonyesha uzito wa Proxima b huenda ukawa
mara 1.3 zaidi ya uzito wa dunia na kwamba inazunguka nyota ya Proxima
katika umbali wa kilomita milioni 7.5. Huchukua siku 11.2 kumaliza
mzunguko mmoja
.
- Proxima Centauri ni ‘nyota nyekundu mbilikimo’; ni ndogo na pia haina joto sana kama Jua
- Inakaribia zaidi lakini kuna uwezekano ikawa imeunganishwa kwa mvuto na Alpha Centauri A & B
- Kwa mtu anayetumia jicho lake kutazama juu angani Alpha Centauri A & B huonekana kama nyota moja
- Sirius A ndiyo nyota inayong’aa zaidi na inayotambulika kwa urahisi zaidi angani usiku
- Jupiter ndiyo sayari kubwa zaidi mfumo wetu wa Jua. Iwapo ingelikuwa na uzito mara 80 zaidi ya sasa, basi ingegeuka na kuwa jua
0 comments:
Post a Comment