Pages

Subscribe:

Sunday, 7 August 2016

TIBA YA ASILIA KUZUIA UGONJWA WA KUHARA


Ugonjwa wa kuhara
Kuhara ni katika magonjwa mabaya ya tumboni ambayo huwapata binadamu na hata wanyama. Mgonjwa asipopatiwa dawa hudhofika kwa kipindi kifupi na hali hiyo ikishamiri humpelekea mgonjwa hata kupoteza maisha.
Mizizi ya Mbono ni dawa nzuri sana ya kukata ugonjwa wa kuharisha kwa aina yoyote ile. 
Chukua ule mzizi mkuu wa mbono, ule unaoelekea chini katakata uloweke kwenye maji safi na salama yaliyo vuguvugu kwa muda wa masaa 3.
MATUMIZI:
Kunywa glasi moja kwa kutwa mara 3, tumia dawa hii mpaka upone yaani uache kuhara. 
Dawa hii pia inawafaa hata wanyama wafugwao kama ng'ombe,mbuzi na kondoo kwa maradhi ya kuhara

0 comments:

Post a Comment