Bab Tale akishuka ngazi za mahakama.
Mkubwa Fela na Bab Tale baada ya kutoka chumba cha mahakama.
Shehe Mbonde anayemshitaki Bab Tale akiwa eneo la mahakama. Kushoto ni wakili wake.
Shehe Mbonde na wakili wake wakishuka ngazi za mahakama.
HUKUMU ya kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale, ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mpaka Septemba 12, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Mustapha Sian alisema sababu kubwa ya
kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kwamba aliyetakiwa kuitolea hukumu ambaye
ni Msajili Projest Kahyoza hayupo mahakamani kikazi.
Katika kesi hii Babu Tale, pamoja na
mdogo wake anayeunda kundi la Tip Top Connection wanatakiwa kuieleza
mahakama kwa nini wasifungwe jela ama kumlipa Shehe Mbonde kiasi cha Sh.
Milioni 250.
source:gpl
0 comments:
Post a Comment