Arsene Wenger amesema Zlatan Ibrahimovic ni mchezaji bora lakini umri wake utampa wakati mgumu Manchester United
Wenger amekiri kuwa hana uhakika jinsi gani Ibrahimovic atachukuliana na soka la Uingereza, kulingana na presha itakayomkabili nyota huyo wa zamani wa Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona na PSG kuipatia magoli Manchester United.
"Kwa kweli sijui jinsi gani ataweza," Wenger aliwaambia waandishi. "Kulingana na kiwango chake, kipaji, ana nia ya kufanya vema. Kitakachopingana naye ni kwamba si mchezaji mdogo tena, hivyo hilo ni swali la kujiuliza kama ataweza kufanya vizuri kila mechi.
"Kulingana na jinsi nilivyomuona mwaka jana Paris Saint-Germain, ulikuwa ni msimu wake uliokamilika zaidi. Alikuwa mchezaji hatari sana msimu uliopita.
"Kwa upande wa ushawishi, ataleta mabadiliko Man United. Ni mshindi, karisma yake itaiimarisha timu na mchezaji mmoja mmoja."
Ibrahimovic huenda akaongoza safu ya mashambulizi ya timu hiyo katika mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Leicester City.
0 comments:
Post a Comment