Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amekiri
kuwa "hatimaye" klabu yake imefanikiwa kuipata huduma ya Paul Pogba
kutoka Juventus
Mustakabali wa Pogba ulikuwa umezungukwa na tetesi nyingi mno majuma ya hivi karibuni, kwa nyota huyo kusajiliwa kwa ada ya kuvunja rekodi na Mashetani Wekundu.
Uthibitisho rasmi ulipatikana leo kutoka klabuni hapo kwamba Mfaransa huyo amepewa ruhusa na Juventus kuendelea na vipimo Manchester, lakini Mourinho ameonya kuwa hana uhakika wa namba katika kikosi chake.
"Pogba? Hatimaye, ni mchezaji mahiri. Mchezaji mzuri kama yeye atakuwa pamoja nasi, hatimaye tunaye," alisema Mourinho.
"Hatimaye tunaye. Anaungana na kikosi cha ushindi. Lakini atalazimika kufanya bidii nyingi kuingia kwenye kikosi. United ni klabu sahihi ambayo itamweka kwenye viwango anavyohitaji kuwa.
"Nimemwona Pogba akikimbia, akicheza kikapu, hufanya kila kitu, kwahiyo natumai atakuwa fiti. Nitakuwa nikimsubiri Jumanne."
Mourinho amenyanyua taji lake la kwanza kama meneja wa United kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa Wembley Jumapili mchana.
0 comments:
Post a Comment