Sasha Obama akihudumia mgahawani.
IKIWA imebaki miezi miwili tu
ili utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama ufikie ukomo, binti mdogo
wa rais huyo mwenye asili ya Kenya, Sasha Obama ameamua kuacha ‘starehe’
za Ikulu ya White House na kuondoka kwenda kufanya kazi katika mgahawa
mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Sasha mwenye umri wa miaka 15 ameanza
kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s
Vineyard, Massachusetts na picha zilizopigwa zinamuonesha akiwa amevalia
sare za kazi za hoteli hiyo na akifanya kazi.
Sasha Obama.
Binti Sasha ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Menu ya mgahawa huo.
Taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo zinaeleza kuwa familia ya Rais Obama hutembelea eneo hilo mara kwa mara wakati wa likizo.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo
aliambia gazeti la Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na
watu sita walikuwa wanamlinda binti huyu, lakini baadaye tukagundua
alikuwa nani (mtoto wa rais Obama).”
0 comments:
Post a Comment